WATOTO LIKIZONI

Nakumbuka mimi nikiwa bado sklini, nilithamini likizo kulikohata masomo kabla ya likizo. Hata hivyo likizo yangu haikuanza rasmi mpaka nimemaliza kazi ya ziada ambayo mwalimu wangu alikuwa amenipea. Hata hivyo lazima nikubali kwamba siku zote nilitangulia na kazi ya zuada ya Kiswahili kwanza kabla ya kukumbuka kwamba pia kulikuwapo na masomo mengine. Waama siku njema huonekana asubuhi. Sasa hivi nchini Kenya, Tanzania na kwingi tu, wanafunzi wako likizoni! Mambo tunayoripotiwa katika uga wetu huu wa msisimko wa Kiswahili ni ya kushangaza kama si kustaajabisha….Yatendelea


6 Responses to “WATOTO LIKIZONI”

 1. Ama kweli Chanda chema huvishwa pete, Mwalimu Msonobari bila kutia chumvi bidii na nidhamu njema uliyonayo ndiyo ilfanya uimarike zaidi katika mambo yote uyafanyayo na hata kutambulika kote duniani. Wozazi wengi wameweza kuwaachilia tu watoto wao bila ya kuzingatia maisha yao ya siku za usoni kwani wanasahau kuwa, mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo.

  Like

 2. Wakati wa likizo ni wakati shamrashamra tofauti. Mwezi wa nne huwa msimu wa Pasaka, mwezi wa nane huwa na sherehe za tohara katika baadhi ya mikoa hapa nchini, na Desemba huwa msimu wa siku kuu ya Krismas. Wakati wa likizo ni wakati ambao wazazi wengi pamoja na wanafunzi huzembea. Hivyo basi inawawiya vigumu kushughulikia masomo. Shukran bingwa kwa utafiti wako. Naamini kuwa walimu na wazazi watashirikiana katika kuboresha elimu ya wanafunzi wao wakati wa likizo. STEPHEN, KIMT.

  Like

 3. Ni wakati wa likizo ya Agosti. Agosti 4, ni wakati wa kura ya maamuzi. Wazazi wote tafadhali wawalinde na wawatunze wanao. Wanafunzi nao wajibidiishe kwa shughuli za masomo. Naamini kuwa hii tu njia ya kipekee ya kukabiliana na utundu wa chipukizi hawa. Kwa sasa wamelikizwa.

  Like

 4. kongole ustadhi kwa elimu yako wakati huu wa likizo kwa wanafunzi.

  Like

 5. Shukrani galacha kwa kugundua uzembe wa wanafunzi wakati wa likizo.
  Natumai hii ni changamoto kwa wazazi pamoja na wanafunzi. Walimu wahakikishe kuwa wanafunzi wanawajibikia masomo ya ziada nao wazazi wasiwape wanafunzi muda wa kufanya maziara.
  Heko bingwa.

  Like

 6. Hapana shaka wako likizoni na watayazingatia maoni yako. shukrani.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: