UNATUMIA VIPI UJANAJIKE WAKO?

Nimezaliwa katika familia ya akinadada wengi sana. Binti azizi mmoja, dada wanne, mama mmoja, nyanya wawili, halati chungu nzima na shangazi wasiohesabika! Wote hawa wamenipa fursa na nafasi ya kuwajua na kuwasherehekea jinsi ambavyo walivyo. Licha ya ufanisi mkubwa wa kielimu, kimaisha, kisiasa, kiuchumi ambao kizazi hiki cha Hawa kimefaulu kupata, bado hawajapoteza ujanajike wao. Bado hawana kiburi na utundu wa wanawake wengine ninaokutana nao vijijini,mijini na majijini mbalimbali.

Bado hawana kiburi na utundu wa wanawake wengine ninaokutana nao vijijini,mijini na majijini mbalimbali.

Kila mwanamke ana haki ya kuwa mwanamke na si kujaribu kuigaiga wanaume ambao anakutana nao katika pilkapilka za maisha kila siku. Nyimbo zenye ukasumba wa kizungu zimeimbwa kwa vinywa vipana na zikasema kwamba, “ Kile ambacho mwanaume anaweza kufanya, mwanamke anaweza kufanya bora zaidi.” Hata hivyo ukweli ni kwamba mwanamke uyo huyo anaweza kufanya hayo yote lakini akiwa mwanamke na siyo akiwa amevalia guo la mwanamume.

Mwanamke anaweza kufanya mambo mengi sana lakini akiwa bado mwanamke na siyo kujibandika ujanadume na ugumu wa mwanamume.

Kwa maoni yangu wakati umefika wa wanawake wote kutambua kwamba wanaweza kufuzu na kufaulu katika kila wafanyalo na wasemalo hata wakiwa wanawake. Isitoshe wanavyo sifa teule ambazo wakizitumia  basi wataweza kuathiri ulimwengu wote kwa mazuri na uzuri bila ya hata mwanamume mmoja kuwahi kuwafikia. Kwanza mwanamke anao UREMBO usio na kifani. Akiutumia vizuri na kwa nia nzuri anaweza kuathiri mume wake, mchumba wake, familia yake na hata wafanyakazi wenza kwa njia ifaayo. Pili mwanamke anayo MANENO ya kutuliza na kufariji, kuasa na kushauri, kuelekeza na kuongoza kila mmoja anayetangamana naye. Utungaji wa maneno yake ni wa hekima na busara. Hufikiria kabla ya kusema chochote kwa maana anatambua kwamba kifo na uhai vimo ndani ya nguvu za ulimi. Mwimbaji wa nyimbo za injili aliimba na kusema, “ Ulimi kiungo kidogo, lakini kina matatizo.” Isitoshe mwanamke pia ni MWANAUHUSIANO. Yeye ni kiumbe cha kuunganisha na kupatanisha. Anaamini katika urafiki wa kuinuana na kuanuana katika majanga mbalimbali. Ndani ya ule mtandao wake wa watu anaohusiana nao misaada, mawaidha, michango na hata ushauri unachipukia ambao naye huuchuja kwa akili zake razini na akapata kusaidika pakubwa. Hatimaye, mwanamke ni MPEVU. Mpevu kwa maana ya kwamba yeye huona mbele kabla hata ya mwanamume kuona. Yeye huwa na hisia ya sita. Sauti ya ndani kwa ndani ambayo humwambia kuhusu ubora au ubovu wa kitu au hali fulani.

Kazi ni kwa akinadada wetu sasa kuamua kama wangependa kuuathiri ulimwengu na kuheshimika.

Wapendwa, hivi viungo ndivyo vinavyomweka mwanamke katika mstari wa mbele kuliko hata mwanamume katika kuathiri ulimwengu kwa utofauti mkubwa zaidi tena kwa wema na hisani bila ya kujipendekeza kwa kiburi na kelele nyingi sana ambazo hazifai.

Kazi ni kwa akinadada wetu sasa kuamua kama wangependa kuuathiri ulimwengu  na kuheshimika kama wanavyofanya wanawake wa familia yangu niliotangulia kutaja au kuwa na mamlaka ya kujipendekeza na kupuuzwa kote.


22 Responses to “UNATUMIA VIPI UJANAJIKE WAKO?”

 1. Wanawake huwa wanapitia mambo mengi duniani, haswa katika familia. Napenda picha hizi za akina dada. Wanadada kotekote wanazidi kuheshimiwa sababu ndio wanaosimamisha familia, jamii, jammaa, marafiki na nchi yote kwa jumla.

  Like

  • Nashukuru sana Binti Vayoleti kwa hayo haswa changamoto uliyowapa wanawake kuhusu kusimamisha familia zao na kupata heshima kutoka kwa wengine kutokana na matendo, maneno na hatua watakazozipiga. Inshallah! Nashukuru sana. Wanawake Hoeee!!!

   Like

 2. Ukielimisha dada, waelimisha dunia nzima!

  Like

 3. Ukisoma Methali 14:1, maandiko yanasema “Nyumba hujengwa na busara ya mwanawake, na vilevile hubomolewa na upumbavu wake.” Ustadhi, wasia wako kwa kinadada wetu utawafaa pakubwa. Shukrani bingw.

  Like

 4. Ustadhi picha za kina dada hawa zimewatoa warembo kupindukia. Urembo wa nje hudhihirisha urembo wa ndani. Naamini kwamba maneno yako mateule yanamchango mkubwa kwa mabinti wote watakao soma blogu hii. Hongera mwalimu.

  Like

 5. Allumin Mazrui katika tamthilia yake ya kilio cha haki ameandika “ulimi ni kisu hukata na vilevile ni sabuni husafisha.” Naye Ken Walibora Waliaula katika riwaya yake ya siku njema akasema “uchawi wa mwanamke ni ulimi wake. Na adabu ndiyo hirizi tu ambayo inaweza kuhani dhidi ya uchawi huo.” Mwanawake ni mwongozo wa jamii na familia kwa ujumla. Kwa hivyo UREMBO, MWANAUHUSIANO, MPEVU na MANENO ya kutuliza na kufariji ni sura ya mwanamke. Shukran Galacha.

  Like

 6. Ushaufu si heshima ya mwanamke. Wasemao husema. Pia wakasema kuwa uzuri wa mwanamke si urembo, ni tabia. Changamoto yangu kwa walofa ni kuwa jamii inawategemea na kila walifanyalo wakadirie kabla ya kutenda. Shukran.

  Like

 7. Ni ukweli kwamba kile mwanamume anaweza kufanya, mwanamke anaweza kufanya bora. Lakini si lazima ajibadilishe kama mwanamume ndo afanye bora. Kina dada wengi siku hizi wanavalia taiti ambazo zinatutia soni. Tafadhali kina wetu tumieni ujanajike wenu vyema. Kila la heri warembo wetu. Wasalaam.

  Like

 8. Ujanajike una panda shika chungu tele. Kwanza kabisa kuufanya uamuzi huwa mlima. Punde tu baada ya kila uamuzi majuto huzakaa. Kina dada, kumbukeni maneno ya busara ya mwalimu, “Mpanda mchongoma, kushuka ndiyo ngoma.” Tafakarini haya. Buriani.

  Like

 9. Wanadada wote wanastahili kupewa nafasi sawa kama mtu yeyote mwingine, maanake wasingukuwepo basi tusingekuwa na kizazi chochote kile.Heko kwa kina dada wote ulimwenguni.

  Like

 10. Ustadhi, kongole kwa elimu yako. Ukweli wa mambo nikuwa, si lazima wanawake wawe na mienendo kama ya wanaume. Ili kuwa mwanamke mwenye hekima ni lazima atakase hulka zake. Kina dada walio na bahati ya kupitia blogu hii mambo hayatawaendea mvange. Asante. STEPHEN, KIMT.

  Like

 11. kwa kweli mwalimu mpasua, wewe ni bingwa kabisa. wanawake wapapaswa washangiliwe na wapewe motisha. wanafaa sana katika ulimwengu tuliyomo. wanastahili hongera kwa mengi waliyoyafanya

  Like

 12. Hewaa… Ushaufu so sifa ya kike. Wasemao husema. Kinadada wenye hulka zisizohitajika hii hapa fursa ya kujinasua kutoka kwa mtego huo. Heko mwalimu.

  Like

 13. Ombi langu kwa kina dada hususana wa hapa jijini Nairobi, ni mavazi. Wengi wa kina dada wetu wanavaa mavazi yasokuwa ya heshima. Tafadhali1i tuonyeshe heshima.

  Like

 14. kiswahili ni lugha yetu hyivo basi tunayo kila sababu ya kukihenzi na kukitukuza.

  Like

 15. Mie najivunia kuwa mkenya kwa sababu ya kiswahili. Nawashukuru wakenya walojitokeza na kuipitisha katiba ambayo inaipa lugha ya kiswahili hadhi yake. STEPHEN KIMT.

  Like

 16. shukrani bingwa kwa wako wasia. STEPHEN, KIMT

  Like

 17. Angalau bingwa makala yako yametusaidia kiasi. Hii ina maana kuwa wameimarika kiulika, japo mavazi yangali yanatisha. Kila la heri bingwa.

  Like

 18. Ujana bila lugha ya kiswahili ni ujana hafifu. Apingaye nani?

  Like

 19. Kazi nzuri. Heko

  Like

 20. Nashukuru sana dada vayoleti kwa hamasa uliyotoa kwa wanawake. Kwani wadada wengi wameshikilia ule mtazamo kwamba wanaume ndio kichwa cha familia. Mtazamo huu ni batili kwasababu wanawake wanaweza bila kuwezeshwa na wanaume kwa kujenga ushirikiano mzuri ktk swala la maendeleo. Pia wanawake wakisimama imara wanaweza kufanya vitu bora zaidi kuliko wanaume. Wanawake tushikamane tukomeshe mfumodume.

  Like

 21. mmmmmhhh, sisemi kitu

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: