MTINDWA YABOMOLEWA USIKU WA MANANE

Kwenye usiku wa kuamkia leo Alhamisi, wafanyibiashara kwenye eneo la Mtindwa jijini Nairobi wameamkia vilio na masikitiko kwa kubomolewa vibanda vyao vya kazi. Eneo la Mtindwa liko kando ya barabara ya Outering kwenye mashariki ya Nairobi katikati ya mitaa ya Buruburu na Umoja.

Kulingana na mama mmoja mwuzaji wa nyanya, ubomoaji huu ulianza mnamo saa nane asubuhi na yamkini askari wa Baraza la Jiji la Nairobi ndio waliotekeleza hayo. “Mimi nilipigiwa simu na rafiki yangu saa nane na robo. Ariniabia kwaba vibanda zetu zinabomolewa. Hata ni bahati mzuri sikukuwa nimezima simu yagu wakati akinipigia,” Mama huyo aliyeshikwa na ghadhabu alinielezea nilipomhoji kwenye macheo ya leo katika eneo lilo hilo la Mtindwa.

Miongoni mwa wafanyibiashara walioathirika pakubwa ni wauzaji mboga na matunda,nguo aina mbalimbali, samani au fenicha, mbao, magari na hata vifaa vya ujenzi. Inaaminika kwamba kumekuwa na vuta nikuvute ya muda mrefu kati ya wafanyibiashara hawa na Baraza la Jiji la Nairobi. Wafanyibiashara wanadai kwamba hawakufahamishwa kwa vyovyote vile kuhusu ubomoaji huo.

Walipokuwa wakijikusanya kwa makundimakundi kando ya mabaki ya vibanda vyao, lori kubwa la askari polisi likiwa limejaa polisi liliwasili mahali hapo na kuwatawanyisha mara moja. Mpaka sasa hakujawa na vurugu lolote lakini hali ya sintoifahamu inazidi kutanda. Inaaminika kwamba, maelfu kwa maelfu ya hela hupatikana kutokana na mauzo ya bidhaa mbalimbali katika eneo hili kila siku!

Wote walioshuhudia hayo walipokuwa katika harakati zao za kuelekea kazini, wamepinga vikali hatua hiyo na kushauri kwamba sote tunafaa kupewa nafasi ya kujiendeleza kiuchumi ili kupiga teke umaskini na athari zinazokuja nao. Katika kuonyesha kwamba maisha lazima yaendelee, wafanyibiashara wengine walikuwa tayari  wamenza kuuza tena bidhaa zao katikati ya sokomoko hilo!

Ama kwa kweli mnyonge hana haki na kama anayo ni mwenye nguvu kupenda. Msongomano wa magari katika barabara hiyo ya Outering ulikuwa mkubwa ajabu huku kila mpita njia akisikitikia hali hiyo ya hasara iliyowakodolea macho.

Waliobomolewa vibanda walionekana kukusanya mali yao kwa simanzi tele pamoja na vifaa walivyokuwa wametumia kujenga vibanda hivyo. Wengine walitunduwaa na kupigwa na butwaa chakari na kubaki wamesimama. Kuketi mtihani, kutembea kibarua! Wenye uwezo zaidi waliyakomboa malori na matrekta na kuvisafirisha vitu vyao kwingineko kwenye usalama zaidi. Wengi hawakujua ni wapi wataanzia na ni wapi watamalizia.

Walaghai na wapora mali hawakusinzia pia katika tukio hilo la kuamkia leo. Inaripotiwa kwamba mali kadhaa ya wafanyibiashara hao waliobomolewa vibanda yamepotea ghafla na hayajulikani yalipo. Hususan wale wanaouza samani au fenicha. Wanadai kwamba zipo baadhi ya samani zinazobebeka kwa urahisi kama vile sofa, meza, viti, vigoda, na kadhalika ambazo hazionekani.. Wizi wa mali na hela wakati wa vurugu ni hali ambayo inafaa kukashifiwa kabisa kwani haifai tutegemee vya ndugu zetu bali tujitahidi na kujitafutie vyetu. Tukumbuke kwamba mtegemea cha nduguye hufa maskini.

Wakati haya yote yakiendelea dada Immaculate, mkazi wa mtaa wa Umoja aliyekuwa amepiga oda ya fenicha kadhaa za nyumba yake mpya, na hata kutoa arbuni  au pesa za mwanzo, anayo wasiwasi kama ya mwasi kuhusu kama ataweza kupata fenicha zake au pengine kurudishwa hela zake. Hata hivyo wafanyibiashara wa samani wamethibitisha hayo na kusema kwamba wote waliopiga oda ya fenicha mbalimbali wataweza kuzipata bila tashwishi yoyote kutoka katika vituo vyao vingine kwingineko.

Ni kweli kwamba sheria ni msumeno, yakata mbele na nyuma. Hata hivyo katika kutekeleza sheria nadhani ni muhimu kujali maslahi ya wengine na kuheshimu sehemu wanazozumbulia riziki kwani michango yao inachangia katika kuimarika kwa uchumi mashinani na katika taifa zima kwa ujumla.

Makala yameandikwa na Mpasua Msonobari,

Languages Africa, Nairobi-Kenya

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI…Asante.


19 Responses to “MTINDWA YABOMOLEWA USIKU WA MANANE”

 1. this is not good at all.the gap between the rich and the poor is widening in kenya and this makes nairobi one of the most dangerous cities in the world.

  Like

 2. Hakika nimesadiki maneno hayo bila makeke.Ni huzuni kubwa pamoja na kicheko kidogo ambacho hakifai

  Like

 3. What a shame! While infrastructure development is important, livelihood development is more important and should also be guaranteed! Thanks for this update!

  Like

 4. ARE YOU SERIOUS!!!!!!!!! I saw it coming. They had been talking about it for a long time now. But they seriously need to expand that road, maybe its for the better for some of us, but I feel sorry for the business people who were there. Kiswahili chako ni poa! It reminds me of Siku njema by Ken Walibora.

  They will obviously not take this sitting down.

  Like

  • Mpasua, hizo picha zapendeza kweli! Yani ustaadi wazo na jinsi zilivyochukuliwa wala sio huko kubomolewa. Nasikitika sana. Sasa kuenda Tuskys Buruburu nikukata tuu! Kazi bora Mpasua. Asante.

   Like

 5. Walipewa notisi kweli? Maanake yaonekana kwenye hizo picha kama wachuuzi hawakutarajia mbumburusho huo. KENYA…!

  Like

 6. It’s so unfortunate esp when it comes to destruction of business.To be honest,i wouldn’t laugh at them but to give them a hopeful hand not to let go of all that but to move on and earn even more..I believe there is always a second option to any negative outcome.Msonobari, asante sana kwa makala hayo mazuri na picha za kipekee.

  Like

 7. This a very bad scenario. At least they should have considered where to take them after demolition. The government is rendering more people jobless by engaging is such acts. I thought President Kibaki said “Tufanye kazi tujitegemee”. what happened to that statement? this is simply absurd. Lord have mercy on us.

  Like

 8. Hata vibanda vibomolewe, bado vitajengwa tena. Mara ngapi tumeona haya???

  Like

 9. Inaumiza kuona biashara ya maskini inaharibiwa bila ridhaa, kwa kweli, adui mkubwa wa mwaafrika ni jirani yake mweusi!

  Like

 10. Ni kweli kwamba haki ya mnyonge ni kilio. Pengo kati ya viongozi matajiri na masikini bado ni kubwa sana. Sheria ya Kenya humfunga mwizi wa mwana mbuzi huku mwizi wa Mbuzi akiachiliwa huru. Hata hivyo tujifunze kiswahili kisha tutajivunia wakenya na tutadumisha umoja, upendo na uungwana. Baadaye unyanyasaji na dhuluma zote dhidi ya binadamu zitakwisha. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Stephen Mukangai KIMT.

  Like

 11. Ndugu Msonobari, ni kweli kuwa vita vya panzi furaha ya kunguru. Wezi husherekea wakati wenye mali wanapoangaishwa. Lakini ni muhimu waelewe kuwa malipo ni hapa duniani, mbinguni hesabu tu. Hata hivzo, Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Stephen Mukangai KIMT.

  Like

 12. Waswahili wanatuambia kuwa aliyezoea vya kunyonga na vya kuchinja hawezi. Waporaji hawa pamoja na wanyanyasaji wote wafahamu fika kuwa siku za mwizi ni arobaini. Na zikizidi arobaini, zitawatokea puani. Hata hivyo kwa wenye haki ujumbe ni kuwa; Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Kwa waso haki ujumbe ni kuwa; Mui huwa mwema. Kongole bingwa kwa habari zako za maslahi. Stephen Mukangai KIMT.

  Like

 13. Asante sana Mwalimu na mjasusi wa Lugha na utafiti kuweza kumulika peupe mazingira tunamoishi, kwa hakika mwenye macho haambiwi tazama ili kila yeyote aliyeweza kuzitama picha hizo, ukweli wote unajitomkeza wenyewe, bisla shaka kitendo kilichotendeka ni cha fedheha zaidi, lakini wafanyibiashara hao wote ilifaa waonyeshwe kiwanja au malahi pa kufanyia pilika pilika zao za kila siku.

  Like

 14. Kongole bingwa kwa kazi nzuri, na pole sana wafanyi biashara wa soko la Mtindwa kwa kupoteza mali yenu. Walaniwe wote wale waliopora mali ya wenyewe. Shukran ustadhi kwa kuangazia yaliyojiri, na matukio yote ujumla. STEPHEN, KIMT.

  Like

 15. Hili ni taifa la Kenya. Wanyonge hawana haki. Naamini kuwa kupitia kwa blogu hii Mungu wa wanyonge atajitokeza na haki yake. Poleni sana wote mliiopoteza mali yenu…

  Like

 16. Aisee bingwa kupitia kwa blogu hii umeweza kutetea haki na nafsi za wanyonge. Natumai sheria itazingatiwa kabla ya hatua kuchukuliwa.

  Like

 17. Kwa sasa katiba mpya haikubali na hairuhusu dhuluma kama hizo!

  Like

 18. ili nchi isonge mbele lazima turudi nyuma kidogo, hiyo ni road reserve na walipewa notice kufikiya friday jioni. walianza kiupewa notice kama meizi sita lakini sonko aka ingiliya

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: