KISWAHILI NI UMASIKINI KWELI

Kiswahili cha karne ya ishirini na moja kinao utajiri mkubwa sana ushindao hata wa dawa za kulevya.  Ukitaalamika kwa taaluma na taalamizi za kiswahili na ujiamni kabisa basi unaweza kupata ukinawiri na kustawi sana. Hata hivyo mambo si mepesi hivyo utakavyodhania ama utakavyotaka kuchukulia.  Yupo rafiki yangu mmoja ambaye huhusisha Kiswahili nao ufalme wa mbinguni. Mavuno ni mengi lakini wavunaji wachache.

Nakumbuka nilipokuwa mdogo nilizoea kutumwa madukani na baba kununua gazeti la Taifa Leo pindi tu babu alipokuja kututembelea. Aliporudi tu kijijini basi pia gazeti la Taifa leo lilirudi mafichoni. Dhana hiyo ilinisumbua sana akilini lakini nikalazimishwa kujua kwamba gazeti la Kiswahili ni la wale ambao hawakusoma na kujaaliwa kujua kusoma kiingereza. Ninayo furaha sana kugundua kwamba dhana hiyo potoshi na aisiyotakikana katu imeanza kusahaulika. Yeyote azungumzaye kiswahili anafaa kujivunia kwa maanani lugha bora na ya kipekee sana ya Kiswahili.

Nionyeshe mtu yeyote aliyefaulu kwa viwango vya dunia na mazingira haya tunayoishi ndani, na nitakuonyesha uswahili ndani yake. Kiswahili si lelemama, aliwahi kusema Mwalimu Nyerere katika hotuba zake kwa watanzania. Leo tunao wandishi wa vitabu vya kiswahili wenye heshima na ulua wao, tunao watangazaji wa kiswahili wenye nafasi za kipekee katika jamii pamoja na walimu wa kiswahili waliobobea katika nyanja ya ufunzaji wa lugha ya kiswahili.Kiswahili kweli ni umasikini?

Swali tunalofaa kujiuliza ni kwamba sisi sote wahusika na wenye kukisarifuu kiswahili tunafanya nini katika kuboresha hali hiyo. Mwanafilosofia mmoja aliwahi kusema kwa uketo na ufasaha kwamba tusiulize kile nchi hii inaweza kutufanyia bali kile ambacho tunaweza kuifanyia  nchi hii.


8 Responses to “KISWAHILI NI UMASIKINI KWELI”

 1. Ustadhi, ukweli wa mambo ni kuwa Kiswahili ni chimbuko la utajiri. Wengi waliofanikiwa kuna uswahili ndani yao. Na wale waliohasi lugha ya kiswahili wanaishi maisha ya uchochole, maisha ya kula chakula fumanizi, maisha ya kulalia ngumi na kujifunika ngumi. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. STEPHEN, KIMT.

  Like

 2. Kiswahili ni lugha ajiri. Wengi walioajiriwa kupitia kwa lugha hii ya taifa wanaishi maisha ya kifahari na ya kupigiwa mfano. Kwa mfano taja jina; Mwalimu Mpasua Msonobari, Guru ustadhi Wallah Bin Wallah, Ken Walibora, Ben Mutobwa, Ustadhi Shaaban Robert{marehemu}, Almin Mazrui, P.L.O LUMUMBA, Mwalim Julius Nyerere, na wengineo. Orodha ni ndefu sana. Hawa ni watu na sifa zao. Wamebobea/walibobea. Wamefanikiwa. Wote ajira yao moja, KISWAHILI. Kwa hivyo kiswahili si umasikini, ni utajiri. STEPHEN, KIMT.

  Like

 3. Kiswahili sio lugha masikini. La! Kiswahili kina utajiri wa kudumu. Kila unapoongea kiswahili sanifu unapata umarufu kushinda tajiri, hivyo basi mwanalugha mkwasi wa mali, utu na ukarimu. Muulize Guru Ustadhi Wallah Bin Wallah atakuambia…

  Like

 4. Sasa ni lugh rasmi. Kwa maana hii utajiri u mikononi mwetu. Ni wajibu wetu tujitolee na tujitume ili kuupata utajiri huu.
  Heko bingwa.

  Like

 5. Kiswahili ni lugha tajiri na ajiri.

  Like

 6. Napinga kwa dhati kuwa Kiswahili ni Umaskini. Ni wazi kuwa ufasaha wa Lugha teule ya Swahili una manufaa makuu. Mradi tu, utilie maanani kutia makali na kuboresha lugha kwa bidii yako mwenyewe. Mwishowe utapta kuwa umeimarika na kunawiri kama mmea ulitiwa samadi.

  Mie,
  Mpenzi Mkuu wa Lugha Teule ya Swahili.
  Ofisa Miguel

  Like

 7. lazima tukitikuze kiswahili na kujivunia.Huu ni utambulisho wetu. kama tutakikana,ni sawa na kukataa asili yetu.Tukikubali kukidharau kiswahili na kushadadia lugha za magharibi tujue wazi ni sawa na mtu asiye na kosa lakini anaamua kujipeleka gerezani mwenyewe.Yaani kuusujudia ukoloni hata kama kwa maneno yetu tunaulaani.

  Like

 8. kweli guru usijiulize hii nchi itakufanyia nini mbali nitafanyiani hii nchi.kusema lugha kwa uketo na ufasaha ni nguvu na utajiru mkubwa.wanao husisha kiswahili na umaskini ni wazungu weusi.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: