KISWAHILI MHIMILI WA MAPENZI

Ama kwa kweli lugha ya kiswahili ni mhimili wa mapenzi.Mhimili kwa maana gani? Mhimili kwa maana ya nguzo au msingi. Mapenzi yoyote yale yanahitaji kukita mizizi baina ya wale wahusika wake. Hukita mizizi tu kama wahusika wake nao wanawasiliana na kusemezana. Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita nilishirikishwa na kampuni moja iitwayo Sasafrica Productions katika kipindi cha kiswahili kilichoitwa Tusemezane. Kipindi hiki kilirushwa mtandaoni na kusikilizwa ulimwenguni kote. Kilisikilizwa na wengi na kipindi kingekosa kurushwa hewani tungejibu mashtaka na lalama chungu furiko. Funzo kuu nililopata kipindini humo ni kwamba kumbe kusemezana ni muhimu na kusemezana kukosekanapo katika uhusiano wa kimapenzi basi mhimili mkuu huwa umeregea regerege na kudondoka kwa mapenzi hayo  kutoka mioyoni mwa wahusika ni rahisi sana kama pera lililoiva kutoka kwenye mpera.

Ukosefu wa kusemezana katika uhusiano hufanya mapenzi kudondoka kutoka kwenye mioyo wa wahusika kama ambavyo pera lililoiva hudondoka mtini

Nakumbuka binti mmoja kati ya wahusika katika kipindi hicho, Nana Vayoleti akisema kwamba mawasiliano na kusemezana hufaulu kwa wale ambao hufaulu katika kuyaendeleza. Nadhai yote hayo ni kweli kwani ukweli wa maisha ni kwamba jinsi tunavyowasiliana na wengine pamoja na kuwasiliana baina yetu sisi wenyewe huchangia pakubwa katika ubora wa mapenzi yetu na hata maisha yetu.

Mawasiliano haya na kusemezana huku vyote havipo bila chombo kizuri cha kusafirisha mawasiliano hayo ambacho ni lugha hususan lugha ya kiswahili.  Zipo sehemu na zipo hali mbalimbali ambazo nimejipata ndani hapo awali ambapo kama kisingekuwa kiswahili changu kilichonipa nguvu za mawasiliano basi nakwambia na kukuhakikishia kwamba mambo yangekuwa yameniendea mrama kwelikweli! Ningekuwa hoi kwelikweli.Sijijui sijitambui.

Lazima nipongeze akinakaka ambao wanaitumia lugha ya kiswahili kwa ufasaha na uketo unaohitajika kwani kama nyinyi bado kapera, basi haliyenu hiyo itawafaa mno.Itawapeleka mbele sana na wapendwa wenu ambao Mungu Atawajalia mkapata.Kwani ufasaha huo uutumieni katika kuelezea wazi jinsi unavyomwenzi mwandani wako na haswa alivyoumbwa akaumbika. Mbona mwandikie mate na wino upo? Nimekuja kugundua kwamba akinabinti wengi sana wanvutiwa na wazungumzaji bora wa kiswahili na wanafurahia sana kujihusisha na uswahili huo licha ya kwamba baadhi yao hawakielewi fika kiswahili hicho. Hilo ndilo jibu la swali ambalo sasa limekuwa swala kotekote kwamba kwa nini muziki wa nchini Tanzania, bongo, umevuma kiasi hicho. Ule uswahili ndani ya nyimbo zile ndio unaokuwa mhimili wa mapenzi ya muziki uo huo. Ama kwa kweli Kiswahili ni mhimili wa mapenzi.

Naambiwa na duru za kuaminika kwamba wapo wakenya fulani hawalali mpaka wamemsikiliza mwanamuziki wa kike wa kutokea Tanzania kwa jina Ray C.

Ukiwauliza wanakutajia sauti yake, sura yake bila kusahau umbo lake. Mimi nashukuru Mungu Aliyenijalia pia mwanamuziki mwenye sauti ya ninga kwangu, azizi wangu maridhia mwanaharakati maarufu wa haki za watoto na wanawake pamoja mwanamawasiliano wa kipekee mno.  Binti mrembo upo? Unanipata?

Salaam aleikum!


7 Responses to “KISWAHILI MHIMILI WA MAPENZI”

 1. Nazidi na nitaendelea kumsifu mwalimu, Msonobari kwa ufasaha na ung’amuzi wake, kwa kujitolea kupitia kwa baraste, tofauti ili kuileta ile picha maridhawa kwa wapenzi wenzangu wa kiswahili. Ama kweli wasemavyo wahenga ‘Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga’, ndivyo mwalimu wetu wa Lugha ya Kiswahili, anavyo tuhakikishia kwamba, kukienzi Kiswahili lazima tuwe na bidii ya kuitikia makosa na kujaribu kadri tuwezavyo kukiongea Kiswahili sanifu. Hongera sana Msonobari kwa uchanganuzi wako wa maswala ya Kiswahili pamoja na utenda kazi mzuri. Naye Rabuka bila shaka akunehemeshee nehema na rehema zake, ili upate kuwa na maisha marefu. Shukrani.

  Like

 2. Ustadhi, Shukran Jidan wa Salaam wa barakatu. Lugha ni chombo cha pekee kwa mawasiliano. Mapenzi bila lugha ni sawa na imani bila matendo. Himizo langu kwa vijana makapera ni kwamba; Chambo kwenye ndoana si mtego, bali ni kivutio ikizingatiwa kwamba chambo chema ni baraka kwa mvuvi. Mwalimu, mbinu ya kalamu yako ni bora. Kazi yako ni mbalamwezi. Vijana wapenzi wa kiswahili, tujifunge vibwebwe ili tufanikiwe. Heko bingwa, MOLA awe jicho lako. STEPHEN, KIMT.

  Like

 3. Kongole bingwa. Vidonge visipotiwa mchuzi vitahitaji ujuzi kumeza. Kiswahili ni mhimili wa mapenzi. Kiswahili ni barabara ya ufanisi. Kiswahili kinastahili kutukuzwa, kisifukuzwe. STEPHEN, KIMT.

  Like

 4. Kiswahili ni rotuba ya aina yake kwa makuzi ya mapenzi. Wanadada wengi huvutiwa na lugha hii ajiri. Ombi langu ni kuwa kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Stephen Mukangai. KIMT.

  Like

 5. Asalaam alaikum bingwa? Nafaharika sana kwa utafiti na uchanganuzi wako. Vilevile kwaniaba ya chipukizi wenzangu wanaoitumia lugha hii patanishi, nasema shukran kwa pongezi zako. Naamini kuwa wasia wako ni rotuba ya pekee uhusiano bora. Kiswahili ni mhimili wa penzi, na vilevile ni chombo cha mawasiliano. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. Wasaalam. STEPHEN, KIMT.

  Like

 6. Bila lugha mapenzi hayatakuwa na ladha. Kiswahili ni nguzo muhimu katika mapenzi.

  Like

 7. Shukrani bingwa kwa ujumbe wako. Naamini kuwa wasomaji watazingatia ujumbe huu kwa uzito wake. Tuulinde uhusiano wetu kupitia kwa lugha hii tamu ya kiswahili.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: