AFCON 2019 Friendlies Egypt Vs Tanzania 1-0 FULL Highlights & ALL Goals June 13, 2019

Hii ilikuwa mechi ya kirafiki kati ya Misri wenyeji wa shindano la AFCON 2019 na Tanzania kutokea Afrika Mashariki watoto wa Magufuli. Ilichezewa kwenye uwanja wa Borg El Arab Jijini Alexandria nchini Misri. Ikumbukwe kwamba uwanja huu ulifunguliwa rasmi mnamo mwaka wa 2005 na ndio mkubwa zaidi Misri na wa pili kwa ukubwa barani Afrika. Unaweza kuingia mashabiki wapatao themanini na sita elfu.

Mechi hii ilikuwa imesubiriwa sana kwa hamu na ghamu huku wengi wakijiuliza kama Misri wataibuka washindi kwenye kombe lenyewe la AFCON 2019 katika msimu huu.

Misri ndio wanaoshikilia kombe hili la AFCON na watakuwa wakijiandaa kulitetea vikali. Mafarao hawa wamelishinda taji hili mara 7 huku wakilitwaa kombe hilo mara tatu kwenye uwanja wa nyumbani.

Kwa ajili ya ushupavu wao huu, wengi walitaka kuegemea upande wao hata hivyo Watanzania wakiongozwa na Emmanuel Emenike walijifunga kibwebwe kuudhihirishia ulimwengu kwamba licha ya kutooonekana AFCON tangu mwaka wa 1980 wangali wanaweza na wana nafasi kuu.

Hata  hivyo bahati haikuwa upande wa Tanzania kwani goli lake Ahmed Elmohamady  mnamo dakika ya 64 ndilo bao pekee kwenye mechi lililowapatia Mafarao ushindi. Kipenfa cha mwisho kilipopigwa Misri walikuw a na goli moja nayo timu ya nyumbani sifuri. Mlinda lango Manula alifanya kazi ya ziada kwenye mechi baada ya kuokoa mikwaju kadhaa. Uwanja haukuwa na mashabiki kabisa na viti kote uwanjani vilionekana kuwasalimia wachezaji uwanjani. Tazama hapa yaliyojiri: https://youtu.be/Q_PDfNAbg-k.

Kundi la A na C

Kwenye kinyang’anyiro hiki kinachokuja cha AFCON Misri wako kwenye kundi la A pamoja na timu za Zimbabwe, DR Congo na Uganda. Wapinzani wao kwenye mechi hii ya kirafiki nao, Tanzania, wako kwenye kundi gumu kwelikweli, kundi la C pamoja na timu za Aljeria, Kenya na Senegal.

Bila shaka huu ulikuwa mtihani mkubwa kwa timu yetu hii ya nyumbani dhidi ya mabingwa Misri na hatimaye dakika 90 za mechi zilisema ukweli wake.

Baada ya kuyasoma makala haya, maoni yako ni yapi kuihusu mechi hii ya kirafiki. hasa baada ya Misri kuipuka Taifa Stars ya Tanzania? Ni mechi gani nyingine ya kirafiki ambayo unasubiria kwa hamu!

Kuwa huru kutuambia maoni yako hapo penye sehemu ya comments nasi pamoja na wasomaji wengine tutayasoma na kuyaweka maoni yetu pia katika harakati za kuchangia mada haya kwani, mchango ni kuchangizana!

Kwa habari kemkem zilizohaririwa kwa ustadi na ufundi bila papara wala payukapayuka hapa ndipo.

Subscribe katika Mpasua Msonobari TV, https://www.youtube.com/user/msonobari/videos,  na ubofye alama ya kengele ili usipitwe na habari kama hizi za michezo, habari murua, habari motomoto, habari zinazochipuka, kila siku!

Mimi ni Mpasua Msonobari, nikiripotia Sasafrica Productions, Zanzibar Visiwani.

Usikose kujiunga yani kusubscribe katika Youtube channel yangu – @Msonobari.

Mpasua Msonobari anapatikana katika anwani hizi:
Swahili WordPress: https://msonobari.wordpress.com

YouTube: https://www.youtube.com/user/msonobari/videos

Facebook: https://www.facebook.com/msonobari/

Instagram: https://www.instagram.com/mpasuamsonobari/

Twitter: https://twitter.com/msonobari/

SoundCloud: https://soundcloud.com/msonobari

SoundBetter: https://soundbetter.com/profiles/129686-mpasua-msonobari

LinkedIn: https://www.linkedin.com/in/mpasuamsonobari

Kwa kazi na ushauriano wa Masuala ya Kiswahili:
Piga simu: +254 725 084 032
Baruapepe: msonobari@gmail.com

~ by Mpasua Msonobari TV on June 13, 2019.

One Response to “AFCON 2019 Friendlies Egypt Vs Tanzania 1-0 FULL Highlights & ALL Goals June 13, 2019”

  1. Asante sana kwa makal haya Mpasua Msonobari. Nani kama weye!

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: