Diamond Anatarajia Mapacha kutoka kwa Dada yake Zari

Thumbnail a_Mpasua Msonobari - Diamond Anatarajia Mapacha kutoka kwa Dada yake Zari

Tafadhali jiunge/ subcribe katika YouTube Channel yangu kwa kubofya hapa: https://www.youtube.com/user/msonobari/

Kwa kweli, jina la lakabu SIMBA, hakulipata bure bilashi! Yeye ni Simba kweli!! Kulingana na duru zinazotoka katika nchi ya matoke, Uganda, Simba anatarajia mapacha kutoka kwa dada ya Zari, kwa maana ya binti mmoja wa Kiganda ambaye anaishi Marekani. Kwa mujibu wa mazungumzo kati ya mwanamitandao maarufu wa Kiganda kwa jina Ritah Kaggwa, anayeishi Uingereza, na rafiki yake Dada wa Zari, mpenzi wake wa siri wa Diamond, pafukapo moshi pana moto. Aidha lisemwalo lipo na kama halipo lipo njiani laja.

Inasemekana kwamba mapenzi kati ya Simba na mpenzi wake huyo wa siri wa Kiganda, yamenoga kwelikweli, kiasi cha wao kushinda wakisogoa kupitia kwa chati ya video, kila
mara. Mtoto wa Museveni, anampeza sana Diamond, na amesikika akisema kwamba, yeye hana haja na pesa za Simba, bali anahitaji tu uwepo wake yeye. ‘Company’ yake! ‘Presence’ yake!

Wanaosema wanasema kwamba hata wanapanga kufanya harusi ya kiraia, yani ‘Civil Wedding’ mnamo mwezi wa Mei mwaka huu, ndiposa harusi ile, Diamaond alikuwa amepanga kufanya naye Mtoto wa Kenyatta, Tanasha, mnamo mwezi wa Februari mwaka huu, haikufua dafu.

Mpasua Msonobari_Diamond Anatarajia Mapacha_1 (26)

Habari hizi, bila shaka zitampiga makonde ya kihisia, mwanaurembo wa Kikenya na mtangazaji wa NRG, Tanasha Donna, na kumwacha akiviona vimulimuli akilini. Hata vumbi halijatulia tangu uvumi wa hivi majuzi wa Diamond, mpenzi wake, kuwa katika mahusiano mengine ya kimapenzi. Habari ambazo hatimaye wawili hao, mtu na mpenzi wake Oketch, walizitupilia mbali, kwa ithibati tosha na ushawishi mkubwa ambao haukuacha doa lolote la shaka. Ikumbukwe kwamba Tanasha Oketch, anatokea Ziwa Victoria, eneo atokalo Baba, Raila Odinga, aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi ya Kenya.

Yamkini alipo Diamaond, anaomba sana kwamba haya yote yasiwe kweli, la sivyo, penzi lake na Tanasha litakuwa limeingia doa na toa kwa kweli! Lakini kama uvumi huu
utakuwa kweli, basi Diamond atakuwa sasa baba wa watoto watano! Kama Tanasha Donna naye atakubali kumpa pia Simba mtoto wa sita linabakia jambo tusilolijua, na gumu kung’amua kwa kweli, sawa na kumtafuta paka mweusi kwenye chumba chenye giza totoro. Waama, watoto kama hao, ni baraka na hawana hatia katu, pengine baadhi ya vitendo viwaletao ulimwenguni humu, ndivyo vyenye hatia.

Mpasua Msonobari_Diamond Anatarajia Mapacha_1 (22)

Kwa ewe mwanaume unayenisikiliza, kama ungekuwa Diamond ungefanya nini? Na je, dada unayenisikiliza, weye ungekuwa Tanasha Donna na haya yawe kweli, ungechukua hatua gani? Basi tuambie hapo penye sehemu ya comments na usisahau kusubscribe kwa habari motomoto kama hizi!

#DiamondPlatnumz #TanashaDonna #DiamondTwins #10over10 #TTTT #NRGRadioKE

Usikose kujiunga yani kusubscribe katika Youtube channel yangu – @Msonobari.

Mpasua Msonobari anapatikana wapi?
Swahili WordPress: https://msonobari.wordpress.com

YouTube: https://www.youtube.com/user/msonobari/

Facebook: https://www.facebook.com/msonobari/

Instagram: https://www.instagram.com/mpasuamsonobari/

Twitter: https://twitter.com/msonobari/

SoundCloud: https://soundcloud.com/msonobari

SoundBetter: https://soundbetter.com/profiles/129686-mpasua-msonobari

Kwa Kazi & Mawasiliano:
Piga Simu: +254 725 084 032
Baruapepe: msonobari@gmail.com

~ by Mpasua Msonobari TV on March 30, 2019.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: