Danson Mungatana aliyekuwa mbunge kule Kenya aomboleza kifo cha mkewe Violet Mungatana

Mke wa aliyekuwa mbunge wa Garsen, na vilevile Mgombea kiti cha Ugavana cha Tana River, Danson Mungatana ameaga dunia!

Thumbnail a_Mpasua Msonobari - Danson Mungatana aliyekuwa mbunge aomboleza kifo cha mkewe Violet

Mke huyo kwa jina Violet Mungatana ndiye aliyekuwa Mke wake wa Kwanza. Duru za kuaminika zinasema kwamba Violet Mungatana, alikuwa akiugua ugonjwa wa figo na aliaga dunia wakati akiendelea na matibabu ya usafishaji damu kwa mashine ya figo, katika hospitali ya Coptic, jijini Nairobi. Amekuwa katika hospitali hiyo kwa yapata mwezi mmoja sasa.

Ikumbukwe kwamba Mheshimiwa huyu, kwa siku za hivi majuzi, ameandamwa na masaibu si kidogo. Aliachana na aliyekuwa mke wake wa pili na Misesi na Malkia wa Kenya, mwaka wa 2005, Cecilia Mwangi, ambaye atakumbukwa vyema zaidi kwa kampeini yake ya kupambana na mafunza yani jiggers pamoja na miradi mingine mingi nchini Kenya.

Aidha, hivi majuzi tu, Mheshimiwa Mungatana ametapeliwa shilingi zipatazo bilioni 2 hela ya Tanzania au milioni 76 hela ya Kenya na wajanja walioko huko Nairobi. Na sasa, chambilecho Waingereza, kuuwekelea msumari moto kwenye kidonda, mkewe wa kwanza – Violet Mungatana almaarufu Mama Elsie ametangulia mbele za haki.

Mheshimiwa Danson Mungatana, amebaki kufarijiwa na kulilia kwa mabega ya mke wake wa tatu, ambaye sasa, tuseme ndiye mke wake pekee. Mke huyo ni mtangazaji maarufu katika kituo kimojawapo nchini Kenya, na anaitwa Mwanaisha Chidzuga. Wamejaaliwa watoto wanne, kitinda mimba, kwa sasa, akiwa dogoo kwa jina Amal ambaye kulingana na mama yake, alipozaliwa hakuletea familia sahani wanavyoimba Sauti Sol wa kukohuko Kenya, bali ‘Hot Pot’. Mwanaisha, mkereketwa mkubwa sana wa lugha ya Kiswahili, ni binti wa aliyekuwa Mwakilishi wa Wanawake, kaunti ya Kwale na shabiki sugu wa chama tawala nchini Kenya kinachoitwa Jubilee, kwa jina Zainab Chidzuga.

Naibu Rais wa nchi ya Kenya, Daktari William Ruto, alitoa rambirambi zake akiifariji familia ya marehemu Violet Mungatana na kusema kwamba, nikimnukuu: “Natuma rambirambi zangu kwa familia na marafiki wa aliyekuwa Mbunge wa Garsen, Mheshimiwa Danson Mungatana kufuatia kifo cha mke wake Violet Mungatana. Alikuwa mwanamke aliyejitolea kuihudumia familia yake, mpole na wa kukaribisha wageni. Alitambulika kwa ukarimu wake na moyo wake mzuri. Lala salama.”

Mheshimiwa huyo ‘mla mamba’ , kwa alama za nukuu, kutoka Kenya, ni wakili mtajika na mwanasiasa wa muda mrefu anayekumbukwa kwa kuwasaidia vijana wengi kujikwamua kutoka kwa umaskini kule Garsen na nchini Kenya kwa ujumla. Anavyosema Guru Ustadh Wallah Bin Wallah, katika Dibaji za Maisha, saidia nchi yako, vizazi vitakukumbuka.

Kutoka katika dawati letu la habari hapa Sasafrica Productions, twatoa risala zetu za pole na makiwa kwa familia ya Mheshimiwa.

Mimi ni Mpasua Msonobari, nikiripotia Sasafrica Productions, Zanzibar Visiwani.

#RIPVioletMungatana #DansonMungatana #MwanaishaChidzuga #SautiSol #LalaSalama #RIP

~ by Mpasua Msonobari TV on March 26, 2019.

One Response to “Danson Mungatana aliyekuwa mbunge kule Kenya aomboleza kifo cha mkewe Violet Mungatana”

  1. Kwa habari nyinginezo, tazama mechi yote ya Taifa Stars Tz vs Uganda Cranes Ug |3 – 0| 2019 AFCON EGYPT na ushuhudie tena historia ilivyoandikwa na vipaji vya wachezaji wa Taifa Stars kudhihirika waziwazi: https://youtu.be/txVGUIxi-JY. Usisahau kusubscribe kwa kubofya hapa: https://www.youtube.com/user/msonobari/

    Liked by 1 person

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: