CHAI YAUZWA BENKINI

Leo katika pilkapilka zangu benkini, nimepata fursa ya kuuziwa chai humo ndani. Subiri kidogo, usiyapepeleke mawazo yako haraka sana. Pia usikimbilie kuihukumu benki kwamba imefilisika kiasi cha kuanza hata kuuza chai. Na hata kama ingeanza, wapo wengi sana waliotajirikia kwa kuuza chai! Nilipoiona meza kando ya Msimamizi wangu wa Benki hiyo pia mimi nilidhani nauziwa chai. Hata hivyo, nilipomsogelea yule dada mhudumu aliyekuwa amesimama kando yake ndipo nilipoutambua ukweli wa mambo. Benki nchini Kenya zi mbioni kushindana. Sijui zinashindania nini, lakini ninachojua ni wale wanaoshindaniwa. Wananchi. Katika kuanza kuzungumza na yule dada mhudumu, nilijipata nikiwa na masikitiko makubwa. Maswali yangu yenye nia nzuri yote yakachukuliwa kuwa kwamba ni uzushi na upuzi mtupu. ‘Leo mwatuuzia chai dada? Mie naomba majani chau kutoka Kenya na sukari unitilie vijiko vitatu.” Kimya! Uso wake akaukunja na mdomo akaushumburua utadhania yuko katika mashindano ya watu wenye sura mbaya. Jambo ambalo halikufaa kutokea kwa mhudumu wa umma kama yeye. Niseme kilikuwa ni kinaya yani, kinyume cha mambo chai ile ilifaa kupewa mimi kwa furaha na moyo wazi lakini nilijipata nikiimezameza kwa machungu.

Nilifaa kuelezewa kinaganaga kwa nini ipo pale, kuanzia lini na mpaka lini….yataendelea

~ by Mpasua Msonobari TV on April 6, 2010.

2 Responses to “CHAI YAUZWA BENKINI”

  1. Asante Msonobari kwa kutufahamisha haya.Kweli, chai kuuzwa benkini ni mawazo mazuri sababu kuna benki zingine ambazo zina line refu sana. Sitaji majina!! Ukiwa kwenye line au Queue, unaweza kunywa chai, haswa wakati huu ambao mvua na baridi ni nyingi. Wanaouza tafadhali..tufurahie kazi yetu na kuwachangamsha wateja.

    Like

  2. Hayo ni makubwa bingwa lakini kama unafikiri utakaribishwa Kenya kwa furaha, basi inakubidi ufikirie tena kwani utu wa mwafrika Kenya haupo tena! Hata hivyo, tusipoyabadilisha haya tutawaachia nani? Heko bingwa Mola akutunuku.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: