KISWAHILI NI UMASIKINI KWELI?

Kiswahili cha karne ya ishirini na moja kinao utajiri mkubwa sana ushindao hata wa dawa za kulevya.  Ukitaalamika kwa taaluma na taalamizi za kiswahili na ujiamni kabisa basi unaweza kupata ukinawiri na kustawi sana. Hata hivyo mambo si mepesi hivyo utakavyodhania ama utakavyotaka kuchukulia.  Yupo rafiki yangu mmoja ambaye huhusisha Kiswahili nao ufalme wa mbinguni. Mavuno ni mengi lakini wavunaji wachache.

Nakumbuka nilipokuwa mdogo nilizoea kutumwa madukani na baba kununua gazeti la Taifa Leo pindi tu babu alipokuja kututembelea. Aliporudi tu kijijini basi pia gazeti la Taifa leo lilirudi mafichoni. Dhana hiyo ilinisumbua sana akilini lakini nikalazimishwa kujua kwamba gazeti la Kiswahili ni la wale ambao hawakusoma na kujaaliwa kujua kusoma kiingereza. Ninayo furaha sana kugundua kwamba dhana hiyo potoshi na aisiyotakikana katu imeanza kusahaulika. Yeyote azungumzaye kiswahili anafaa kujivunia kwa maanani lugha bora na ya kipekee sana ya Kiswahili.

Nionyeshe mtu yeyote aliyefaulu kwa viwango vya dunia na mazingira haya tunayoishi ndani, na nitakuonyesha uswahili ndani yake. Kiswahili si lelemama, aliwahi kusema Mwalimu Nyerere katika hotuba zake kwa watanzania. Leo tunao wandishi wa vitabu vya kiswahili wenye heshima na ulua wao, tunao watangazaji wa kiswahili wenye nafasi za kipekee katika jamii pamoja na walimu wa kiswahili waliobobea katika nyanja ya ufunzaji wa lugha ya kiswahili.Kiswahili kweli ni umasikini?

Swali tunalofaa kujiuliza ni kwamba sisi sote wahusika na wenye kukisarifuu kiswahili tunafanya nini katika kuboresha hali hiyo. Mwanafilosofia mmoja aliwahi kusema kwa uketo na ufasaha kwamba tusiulize kile nchi hii inaweza kutufanyia bali kile ambacho tunaweza kuifanyia  nchi hii.

~ by Mpasua Msonobari TV on March 28, 2010.

2 Responses to “KISWAHILI NI UMASIKINI KWELI?”

  1. Surely this is a challenge to many people who dont take seriously, the Swahili Language. There is nothing difficult, everything is possible through, hard work and practice. For you to achieve anything that you do, you must have a positive attitude towards it i.e for you to be famous in Kiswahili language like other eminent persons like Mwalimu, Julius Nyerere, and many more others you should sacrifice, practice and feel free to consult the experts. I give credit to Mr. Msonobari, for his efforts of making sure that the Kiswahili Language is fluently spoken and spread in Africa at large, may God give him strength and wisdom for the good job that he is doing. Thanks.

    Like

  2. Kiswahili ni utajiri, bali si umasikini. Kiswahili ni mila na desturi yetu. Msahau mila ni mtumwa, wasemao husema. Wengi wa watumwa wanaishi maisha ya uchochole. Maisha ya kula chakula fumanizi, kulalia ngumi na kujifunika ngumi. Lakini tajiri wa sasa kuna kiswahili ndani yake. Wengi wa waandishi wa kiswahili na watangazaji mfano wa mwalimu Msonobari, guru ustadhi Wallah Bin Wallah, Ben Mtobwa, Mohammed Said, marehemu Katama Mukangai, Allumin Mazrui n.k. Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe. KISWAHILI SI UMASIKINI. Shukrani bingwa.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: